Rais Kikwete: Sera ya Nje itabakia ile ile
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa siasa ya nchi za nje na misingi mikuu ya kuongoza mahusiano ya Tanzania na nchi za kigeni hayatabadilika hata baada ya yeye kuondoka madarakani.