Watumishi saba wasimamishwa Bukoba kwa ubadhirifu
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera wamewasimamisha watumishi saba wa idara mbalimbali katika halmashauri hiyo ili wapishe uchunguzi zaidi juu ya tuhuma zinazowakabili za kuhusika na ubadhilifu wa fedha za umma.
