Madiwani Misungwi wakanusha kumtetea Kitwanga
Baraza la madiwani Halmashauri ya Misungwi limesema halijawahi kutoa kauli ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba hawakuunga mkono uamuzi wa Rais Dkt. John Magufuli kumfuta kazi aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga.