Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amewataka wawekezaji na wafanyabiashara nchini Tanzania kuwa wabunifu kwa kutengeneza bidhaa zenye ubora wa kuleta ushindani na mataifa mengine duniani.
Balozi Mahiga ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Jumuiya ya umoja wa Mabohora waishio nchini Tanzania ambao walimkabidhi madawati 105 kwa ajili ya shule mbalimbali nchini yenye thamani ya pesa za kitanzania shilingi Milioni 10.
Balozi Mahiga amesema wafanyabiasha wakiwa waaminifu katika uzalishaji wa bidhaa zao wataiwezesha nchi kuwa na uchumi wa kati jambo ambalo serikali ya awamu ya tano inalenga kufikia.
Nae mwenyekiti wa Mabohola nchini Bwana Adam Jee amesema msaada huo wa madawati
ni mwanzo wa mashirikiano baina ya taifa lao na Tanzania.




