Mbunge wa Peramiho Mhe. Jenista Mhagama amefariki dunia leo Disemba 11, 2025 jijini Dodoma.
Taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu imethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuongeza kuwa mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
"Kwa masikitiko makubwa naomba kutangaza kifo cha mbunge wa peramiho Mheshimiwa Jenesta Joakim Mhagama kilichotokea leo 11 Disemba, 2025 jijini Dodoma."
"Natoa pole kwa waheshimiwa wabunge wote, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Peramiho, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu," taarifa ya Spika wa Bunge imesema.
Aidha, taarifa ya Spika Zungu imedokeza kuwa Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaenelea kutolewa.



