Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wananchi wafunga barabara ya Dodoma- Dar

Friday , 9th Dec , 2022

Wananchi wa Kijiji cha Pandambili wilayani Kongwa mkoani Dodoma, wameziba barabara kuu inayotoka Dar es Salaam kwenda mikoa mingine wakishinikiza serikali iweke alama za tahadhari katika eneo hilo baada ya mtoto mdogo kugongwa na gari hapo jana na kupoteza maisha.

Foleni ya magari katika eneo la Pandambili

Mashuhuda wamesema wananchi wamefunga barabara hiyo tangu saa 8:00 mchana wa leo Desemba 9, 2022, hali iliyopelekea kuwepo kwa foleni kubwa ya magari katika barabara hiyo.

Hadi sasa viongozi ikiwemo jeshi la polisi wamefika eneo hilo na wameweza kuwadhibiti wananchi na kuanza kuruhusu magari kutembea.

Juhudi za kumtafuta Mkuu wa wilaya ya Kongwa zinaendelea.