Monday , 20th May , 2024

Mahakama ya Wilaya ya Songwe Mkoani Songwe Mei 20, 2024 imemuhukumu kifungo cha miaka 30 Simon Salati Mwakasula (65) mkazi wa Saza Wilaya ya Songwe kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Chato mwenye umri wa miaka 10.

Gerezani

Mahakama imeeleza kuwa mtuhumiwa alifanya kitendo hicho Februari 09, 2024 cha kumbaka mwanafunzi huyo kwa kumlaghai kwa kumapatia zawadi ya soda kisha kwenda nae shambani kwake na kumbaka.

Kesi ilisikilizwa na upande wa mashitaka ulileta mashahidi watano ambao walithibitisha kosa na mtuhumiwa alitiwa hatiani kwa mujibu wa sheria.

Mbele ya Mhe. Lefi Sizya SRM, Mahakama imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka ili iwe fundisho kwa watu wengine.