Jumatatu , 20th Mei , 2024

Ukosefu wa huduma ya Nishati ya Umeme katika Kata ya Madanga Ng'ambo wilaya ya Pangani Mkoani Tanga umekilazimu Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga kusaidia upatikanaji wa huduma hiyo baada ya kukabidhi kiasi cha shilingi Milioni 8.8 kwa ajili ya kununua nguzo za umeme.

Kwa mara ya kwanza wananchi hao wanakwenda kufurahia huduma ya umeme kwenye eneo hilo baada ya kuikosa tangu kupatikana kwa uhuru. 

Awali akikabidhi kiasi hicho cha fedha kwa mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mussa Kilakala,  Mwenyekiti wa ccm Mkoa Tanga Rajab Abrahaman Abdallah alisisitiza kuharakishwa kwa manunuzi ya nguzo hizo ili wananchi waweze kupata nisgati hiyo. 

Mwenyekiti alisema mara baada ya wananchi hao kutoa kilio chao hivi karibuni akiwa kwenye mkutano wake wa h.adhara katika kata hiyo juu ya ukosefu wa huduma ya umeme aliona ipo haja ya kusaidia ili wananchi waweze kupata nishati hiyo kwa uhakika ikiwa ni pamoja na kujikwamua na umasikini kwa kujihusisha na ujasiriamali unaohusiana na ueme 

"Nikuombe mkuu wa Wilaya nimekukabidhi kiasi hiki cha fedha kwajili ya manunuzi ya nguzo za umeme,  nikusihi sana ukasimamie jambo hili na wananchi waweze kuunganishiwa nishati hii kwa haraka kwani lengo la serikali ni kuhakikisha inatatua kero zinazowakabili wananchi ikiwa ni pamoja na hii ya umeme, 

Wananchi hawa hawahitaji umeme iwa ajipi ya anasa, bali wanahtaji umeme kwa ajili ya maendeleo yao ikiwa ni pamoja na kujiingizia kipato kwa kufanya kazi zinazohusiana na nishati hiyo" alifafanua Mwenyekiti. 

Naye mkuu wa Wilaya ya Pangani Mussa Kilakala aliahidi kusimamia mchakato huo ili uweze kufanyika kwa haraka na wananchi waweze kufurahia huduma hiyo. 

"Sisi kama wasaidizi wako tumefanya kazi kwa kushirikiana na wananchi wa Kitongoji hichi cha Ng'ambo, kuhakikisha ile ahadi yako unakwenda kuitimiza kwa vitendo" alisema Kilakala. 

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Tanga Shaibu Mwanyoka alimpongeza Mwenyekiti na kusema kuwa ni kiongozi huyo amekuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa amekuwa akiguswa na matatizo ya wananchi bila kujali itikadi ya vyama wala ubaguzi wowote kwa watu wote. 

"Haya unayoyafanya leo ni zile kura ambazo kila ukizikumbuka unakumbuka kuwatumikia wananchi hawa bila kusita,  na hii inathibitisha ni kwa namna gani unaguswa na matatizo ya wananchi na hii inadhihirisha wazi hawakufanya makosa katika kukupa zile kura zao za kuhakikisha unawatumikia, "alisema Shaibu Mwanyoka. 

Katibu msaidizi wa Ccm Mkoa wa Tanga Lawrence Kumotola alisema kuwa wananchi hao wanakabiliwa na kero hiyo kwa muda mrefu jambo ambalo chama hicho kimeliona na kuweka nguvu yake. 

"Wananchi hawa walikuwa hawawezi kuchaji simu hata kuchemsha maji kwa kutumia majiko ya kisasa, lakini wewe Mwenyekiti kwa niaba ya chama cha mapinduzi ukasema Mkuu wa wilaya na Tanesco wafike katika eneo hilo na kuwasilisha ofisi za chama.