Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Khamis Kigwangala.
Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya katika hosptali hiyo Mhe. Kigwangala amesema amebaini kuwa kuna upungufu mwingi katika hospitali hiyo hususani kitengo cha maabara pamoja na vitengo vingine
Mhe Kigwangala amesema anashangazwa na hospitali kubwa kama hiyo kukosa huduma muhimu ikiwemo maji pamoja na suala la usafi na huduma ambazo haziridhishi kabisa.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo amesema kuwa serikali iko katika mipango ya kusambaza madaktari bingwa katika mikoa ya pembezoni huku akizitaka mamlaka husika za hosptali kuwaandalia mazingira bora ya kufanyia kazi.