Rose Senyagwa, Mchambuzi wa Masuala ya Hali ya Hewa kutoka TMA
Akizungumza na EATV mchambuzi wa masuala ya hali ya hewa kutoka TMA Rose Senyagwa amesema huenda kimbunga hicho hadi kufikia majira ya usiku kikawa kimekaribia maeneo ya Pwani ikiwemo mikoa ya Dar es salaam, Pwani Lindi na Mtwara ambapo amesema taarifa zaidi zitaemdelea kutolewa kadri muda unavyokwenda
Amesema miongoni mwa kundi linalopaswa kuchukua tahadhari ni wavuvi na wote wanaopenda kutembelea maeneo ya fukwe wanapaswa kuichukua tahadhari dhidi ya uwepo wa kimbunga hicho
Mwisho amewasisitiza wananchi kutodharau au kubeza taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa kwasababu kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Kimataifa la utabiri wa hali ya hewa zinaonyesha taarifa za utabiri zinazotolewa Nchini Tanzania ni za uhakika kwa zaidi ya asilimia 90