Monday , 20th May , 2024

Rapa namba 1 kutoka Ghana Sarkodie ameendeleza vita yake na rappers wa Nigeria akiwaambia levels zake za ushindani ni Kendrick Lamar na J Cole kutoka Marekani.

Picha ya rapa Sarkodie

Sarkodie amefunguka hilo kupitia lines zake wimbo wake wa 'Brag' ambao amemtaja Wizkid, Burna Boy, Davido, Asake na Black Sherif kuwa wamemkuta na amewafanya waanze muziki.

"Wizkid amekuja mimi tayari nafanya muziki, wakati Davido anaanza nilikuwa nisha-prove na Odogwu (Burna Boy) amekuja kupitia Black Sherif mpaka Asake na bado naendelea walidhani nitafeli".

"Washindani wangu wakubwa ni Kendrick Lamar na J Cole" - amesema Sarkodie 

Sarkodie anasema hakuwa na lengo la kuwavunjia heshima kumtaja Wizkid, Davido na Burna Boy lengo ni kuwalenga rapa wajue jinsi gani alivyokaa muda mrefu kwenye muziki.