Jumanne , 21st Mei , 2024

Shirika la Bima la China (SINOSURE) linaendelea na taratibu za upatikanaji fedha za kugharamia ujenzi wa kipande cha tano cha reli ya kisasa (SGR) kutoka Isaka hadi Mwanza chenye urefu wa kilomita 341 na kuonesha nia ya kusaidia upatikanaji wa fedha za ujenzi wa kipande cha sita

Reli

cha ujenzi wa reli hiyo kutoka Tabora hadi Kigoma chenye urefu wa zaidi ya kilomita 411.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Shirika la Bima la China (SINOSURE), ukiongizwa na Meneja Msaidizi wa Shirika hilo, Bi.  Bi Xiaonan.

Dkt. Nchemba amelishukuru Shirika la SINOSURE kwa kuendelea na taratibu za upatikanaji fedha za ukamilishaji wa mradi huo kwa kuwa vipande hivyo ni muhimu katika ukamilishaji wa mradi huo.

"Tumekuwa na kikao kizuri katika kujadiliana ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na China hususani kwenye eneo la ugharamiaji wa miradi ya kimkakati ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha tano kutoka Isaka hadi Mwanza ambapo SINOSURE ilikubali kushiriki katika upatikanaji wa fedha wa kukamilisha ujenzi huo na kipande cha Tabora hadi Kigoma," alisema Dkt. Nchemba.