Picha ya Diddy na Cassie enzi za mahusiano yake
Diddy anasema anamuomba Mungu kwa rehema, huruma na neema zake na kujitolea kuwa mwanaume bora kila siku.
“Sitoi visingizio nimegonga mwamba, Tabia yangu katika video hiyo haina udhuru. Ninawajibika kikamilifu kwa matendo yangu katika video hiyo na kuchukizwa kufanya hivyo”
“Ilinibidi kumwomba Mungu rehema na neema zake, Samahani nimejitolea kuwa mwanaume bora kila siku. Siombi kusamehewa lakini naomba msamaha wa kweli” anasema Diddy
Diddy na Cassie walianza penzi lao mwaka 2007 mpaka walipoachana rasmi Oktoba 2018 lakini Novemba 2023 Cassie alifungua mashtaka ya unyanyasaji, ubakaji na biashara ya ngono dhidi ya Diddy.