Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mashabiki wachelewesha mechi, United na Liverpool

Sunday , 2nd May , 2021

Mashabiki wapatao 200 wa Manchester United wamevamia katika eneo la kuchezea (pitch) la uwanja wa Old Trafford kuendeleza maandamano ya kupinga umiliki wa familia ya Glazer katika klabu hiyo.

Mashabiki wa Man United waliovamia uwanja wa Old Trafford

Tukio hilo limefanyika mapema jioni hii ya leo Jumapili Mei 02, kabla ya mchezo wa Ligi kuu ya England dhidi ya Liverpool ambao ulipangwa kuanza majira ya saa 12:30 jioni ya leo.

Mashabiki hao tayari wameondolewa uwanjani na kikosi cha ulinzi na wengine kuamua kuondoka kabisa uwanjani hapo na kurudi majumbani kwao. Pia kulionekana kuwa na maandamano mengine nje ya hoteli ambayo wachezaji wa Man.United walipumzika kabla ya  kuelekea uwanjani kwa ajili ya mchezo huo.

Maandamano hayo yamekuja baada ya uamuzi wa wamiliki wa United, pamoja na vilabu vingine vitano vya Ligi Kuu ya England, kujiunga na European Super league mapema mwezi uliopita kabla ya vilabu vyote kujitoa katika mashindano hayo.

Mwamuzi wa mchezo huo Michael Oliver na nahodha wa zamani wa Man.United Gary Neville walikuwa miongoni mwa wale ambao magari yao yalizingirwa na mashabiki walipokua wanaingia uwanjani, lkini hadi sasa hakuna taarifa yoyote ya watu kujeruhiwa wala uharibifu wa mali.

Kwa mujibu wa Sky Sports, mchezo huo utachelewa kuanza ili kuhakikisha hali ya usalama inakuwa sawa katika mazingira ya uwanja.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa