Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wabunge wote Tanzania kukaguliwa

Tuesday , 19th Jun , 2018

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imewataka wabunge wote kuwasilisha taarifa za mali wanazomiliki kwa Katibu wa Bunge kabla ya Juni 25, 2018.

Akitoa taarifa ya hiyo ya Sekretarieti leo Naibu Spika Dk Tulia Ackson amesema Sekretarieti ilitoa muda kwa wabunge kuwasilisha taarifa za umiliki wa mali zao na kwamba wabunge wengi hawakutekeleza agizo hilo.

Sekretarieti iliwataka kuwasilisha nyaraka kabla ya Juni 25, 2018 zinazohusu fedha zilizoko benki au taasisi zingine za fedha, hisa, majengo, nyumba, madeni, mashine, viwanda, mitambo, magari na aina nyingine za usafiri, madeni na mikopo kwa mali zote zilizopo nje,” amesema.

Dk. Tulia amewafahamisha wabunge kwamba mwakilishi wa Kamishna atafika ofisini kwa Katibu wa Bunge kuchukua taarifa za wabunge.

Pamoja na taarifa hiyo Dk Tulia amesema kwa kuwa kuna kundi ambalo halikuwa na taarifa kuhusu kuwasilisha vielelezo vya mali zao wataangalia jinsi ya kuwasiliana nao ili kuona vitawasilishwa lini mara baada ya kurudi kwenye majimbo yao.

Naye Mbunge wa Ulanga Mashariki, Goodluck Mlinga (CCM) ameitaka serikali kuhakikisha uhakiki wa mali za wabunge unaenda sanjari na uhakiki wa kiwango cha elimu na taaluma zao.

HABARI ZAIDI

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Wanahabari wasisitizwa kuzingatia maadili ya kazi

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC atangaza msako kuwaondoa walinzi wazee kazini

Rose Senyagwa, Mchambuzi wa Masuala ya Hali ya Hewa kutoka TMA

Kimbunga "IALY" kinazidi kusogea Pwani ya bahari