Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea
Akiongea kwenye mkutano mkuu wa Chama Kikuu Cha Ushirika Cha Songea Namtumbo (SONAMCO) mkuu wa wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile amesema ili kuondoa changamoto ya madeni ambayo inavikumba vyama vingi vya ushirika ni wajibu wa wakulima kurejesha fedha ambazo walikopa kwa ajili ya kilimo.
Vyama vya ushirika ambavyo vipo chini Chama Kikuu Cha Ushirika cha Songea Namtumbo (SONAMCO) vinadaiwa zaidi ya Dola laki 8.63 katika Bank ya NMB na zaidi Dola milioni 1 katika Bank ya CRDB huku madeni hayo yakiwa ni ya muda mrefu zaidi ya miaka 20.
Kwa upande wao wakulima wa Chama hicho wamesema changamoto kubwa ni kucheleweshewa mikopo ya pembejeo hali inayosababisha wakulima kushindwa kuandaa mazao yao kwa wakati.