Mafikizolo wawakubali Watanzania
Kundi la muziki la Mafikizolo ambalo usiku wa Jumamosi limefanya burudani ya aina yake Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mlimani City, wametoa ya moyoni kuwa, wamefurahishwa na kushangazwa na jinsi mashabiki wao hapa Tanzania wanavyowaelewa.