Mashindano makubwa ya kucheza nchini Tanzania "Dance 100%"
Kituo cha East Africa Television Limited kimeandaa shindano kubwa la kucheza mziki lijulikalo kama Dance 100%. Shindano ambalo huwapa nafasi washiriki kutoka pande zote za Tanzania hasa wakiwa katika makundi.Ushiriki unakuwa katika hatua ya mchujo mara tatu na hatimae kufikia robo fainali, nusu fainali hadi kufika fainali.Shindano lote la Dance 100% pia inaonyeshwa katika luninga ya EATV.
