Wafanyakazi Chang'ombe hatarini kuathirika kiafya
Wafanyakazi wa baadhi ya viwanda mbalimbali binafsi vilivyopo Mtaa wa Dakawa,Chang'ombe Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wako katika hatari kubwa ya kupata madhara ya kiafya kutokana na maeneo hayo ya viwanda kuzingirwa na maji mengi, machafu na yenye kutoa harufu.