Dar kuwa na hospitali maalumu kwa wajawazito
Uongozi wa jiji la Dar es Salam umesema uko mbioni kujenga hospitali ya wazazi itakayoweza kuwahudumia wakazi wa wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke kwa pamoja ili kuepukana vifo vinavyotokana na upungufu wa vituo vya kutolea huduma za uzazi.

