Aliyeuliwa na Polisi Njombe, chanzo ni deni
Baba mdogo wa marehemu anayedaiwa kuuwawa kwa kupigwa na risasi na askari Polisi amesema chanzo cha kifo cha mwanae Basi Mwalongo ni kuwa alikuwa anamdai askari huyo na kuitaka serikali ihakikishe inambana mtuhumiwa ili aeleze chanzo.