MOAT yapinga Muswada wa haki ya kupata habari
Wakati wadau wa habari wakikutana leo na kamati ya Bunge wakitaka miswada miwili ya habari isijadiliwe bungeni, chama cha wamiliki wa vyombo vya habari nchini MOAT kimesema kupitia miswada hiyo serikali itavinyima vyombo vya habari uhuru.

