Sekta binafsi imetoa mchango mkubwa sekta ya ajira
Serikali imesema kuwa inathamini mchango mkubwa unaotolewa na sekta binafsi katika kutoa ajira kwa vijana na kusema kuwa itarasimisha sekta hiyo ili iweze kutoa ajira kwa wingi kwa kundi hilo kwani ndiyo mhimili mkuu wa ajira nchini.