Mulamula aapishwa kuwa katibu mkuu Mambo ya Nje
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Mei 27, 2015, amemwapisha Katibu Mkuu mpya, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Rutageruka Mulamula.