Jay Moe: Video zimepunguza ubora wa rekodi
Rapa J Moe, ameeleza kuwa mabadiliko yaliyotokea katika game ya muziki na kuwavuta wasanii kuwekeza katika video zaidi, yameondoa ubora katika kazi wanazofanya na pia kuvuta mashabiki katika kutazama video zaidi na siyo ubora wa rekodi yenyewe.