Serikali yaonya viongozi vyama vya akiba na mikopo
Serikali imewaonya viongozi wa vyama vya akiba vya kuweka na kukopa mkoani Kilimanjaro, kuepuka kuingia katika kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za walala hoi kwa kuwa vitendo vya ubadhirifu ndio chanzo kikuu cha kufa kwa vyama hivyo.