Wafanyakazi wa benki kuchunguzwa kwa uhalifu
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa wapo baadhi ya wafanyakazi wa benki, ambao kwa namna moja au nyingine, wanashirikiana na majambazi kufanya uhalifu; na sasa linawasiliana na wamiliki wa taasisi za kifedha.

