Hakuna fidia kwa wanaobomolewa mabondeni-Mecky
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema watu waliojenga mabondeni wanaobomolewa nyumba zao hawatalipwa fidia ikiwemo kupewa viwanja na kuonya kuacha kuvamia mashamba ya watu kwa kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkuu huyo wa Mkoa Bw, Meck Sadick amesema kuwa wakazi hao wa mambondeni wanapaswa kuondoka wenyewe wasisubiri fidia ambayo haipo.