Stars ni hesabu tu kwa Mafarao taifa hii leo.
Kwenye mpira lolote linaweza kutokea! Huo ni usemi ambao Taifa Stars inaingia nao Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikipiga hesabu kali za kuikabili Misri kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017 zitakazofanyika nchini Gabon.