Baada ya Keshi Nigeria yapata pigo lingine Leo.
Kocha Mkuu wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, Shaibu Amodu amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 58 kifo hicho cha ghafla ni kama kutonesha kidonda cha mashabiki wa soka nchini humo ambao siku chache zilizopita waliondokewa na kocha Keshi.