Jumanne , 19th Jul , 2016

Katibu mkuu wa Wizara ya viwanda,biashara na uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru amezitaka Taasisi za fedha na mabenki kupunguza riba mbalimbali za mikopo ili kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kuweza kukopa.

Dkt.Meru ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam katika zoezi lakuwekeza hati fungani za NMB kwenye soko la Hisa la Dare es salaam DSE ambapo wamewekeza kiasi cha shilingi Bilioni 41.1 ikiwa ni zaidi ya lengo lao la Bilioni 20 pesa ambazo zinapelekwa kwenye miradi ya maendeleo nchini.

Kwa upande wake mkurugenzi wa soko la hisa nchini bwana Moremi Marwa amezitaka taasisi mbalimbali nchini kubdili mifumo yake ya uwekezaji wa pesa za maendeleo.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Banki ya NMB nchini Bi.Ineke Bussemaker amesema Banki hiyo itaendelea kuongeza mtaji katika kuendelea na kuwawezesha wawekezaji na wafanyabiashara nchini kuendelea kutumia fulsa hiyo.