Wanasheria Mahakama ya Afrika kujengewa uwezo
Wataalamu wawili kutoka mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu (ECHR) wako jijini Arusha katika kongamano linalolenga kuimarisha uwezo wa utendaji kazi wa shughuli za Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfHPR).