Jumatano , 20th Jul , 2016

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imewafungia wachezaji watatu, walioshiriki katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL), kituo cha Morogoro 2015/2016.

Alfred Lucas, Afisa Habari wa TFF

Kikao cha Kamati ya TFF kilichokaa Julai 14, 2016 kujadilina kupitia malalamiko na taarifa za waamuzi na kamisaa za mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa RCL kituo cha Mororgoro, kimebaini kwamba wachezaji Imani T. Mwanga, Fred John Lazaro na Brown Chalamila walifanya udanganyifu wa majina ili kukamilisha zoezi la usajili.

KUHUSU MCHEZAJI IMANI T. MWANGA
Kamati imepitia taarifa za waamuzi na kamisaa pamoja na uthibitisho uliopatikana imemkuta na tuhuma za udanganyifu wa jina. Alitumia majina mawili tofauti. Imani Vamwanga ligi daraja la kwanza klabu ya Kurugenzi FC na Emmanuel T. Mwanga klabu cha Stand Misuna.

Kwa mujibu wa kanuni za ligi ya mabingwa wa Mikoa, kanuni ya 39 (1) Kamati imekufungia kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miezi 12. Adhabu hii inaanza toka tarehe ya kuandi kwa barua yake.

KUHUSU FRED JOHN LAZARO
Kikao hicho kimebaini kwamba Fred John Lazaro pamoja na klabu ya Stand Misuna FC walifanya udanganyifu wa majina ili kukamilisha zoezi la usajili.

Kupitia taarifa za waamuzi na Kamisaa pamoja na uthibitisho uliopatikana, imebainika Fred John Lazaro alifanya udanganyifu wa majina hivyo kuchezea klabu mbili tofauti katika msimu mmoja isivyo halali.

Katika klabu ya Stand Misuna FC iliyoshiriki ligi ya mkoa Singida na ligi ya mabingwa wa mikoa kituo cha Morogoro 2015/2016 alisajiliwa kwa jina la Fred John Lazaro kwa usajili namba 044 akivaa jezi namba 13, pia katika klabu ya Singida United FC ya Singida iliyoko daraja la pili (SDL) msimu wa 2015/2016 alisajiliwa kwa jina la Adolf Anthon leseni namba 950725003 akivaa jezi namba 3, 6 na 8 katika mechi tofauti.

Kamati imebaini kuwa Fred siyo mchezaji halali kuichezea timu ya Stand Misuna FC katika ligi ya mabingwa wa mikoa kwa ni hakucheza ligi ya mkoa Singida, na pia kwa kushirikiana na uongozi wa klabu ya Stand Misuna FC amedanganya majina ili kufanikisha zoezi la usajili kinyume cha kanuni ya 48 kipengere cha (2) na (4).

Hivyo kwa mujibu wa kanuni za ligi ya mabingwa wa Mikoa, kanuniya 31 kipengere cha (11) na kanuni ya 39 kipengere cha (1) Fred John Lazaro jezi namba 13 (mchezaji) amefungiwa kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miezi kumi na mawili (12).

KUHUSU BROWN CHALAMILA
Kikao kimebaini kwamba Brown Chalamila pamoja na klabu ya Stand Misuna FC walifanya udanganyifu wa majina ili kukamilisha zoezi la usajili.

Katika klabu ya Stand Misuna FC iliyoshiriki ligi ya mkoa Singida na ligi ya mabingwa wa mikoa kituo cha Morogoro 2015/2016 alisajiliwa na kucheza kwa jina la Costa Bryan Bosco kwa usajili namba 029 akivaa jezi namba 03, wakati ni mchezaji halali wa klabu ya Kurugenzi FC ya Mafinga-Iringa iliyoko daraja la kwanza (FDL) msimu wa 2015/2016 leseni namba 921004001 akivaa jezi namba 03.

Hivyo, kwa mujibu wa kanuni za ligi ya mabingwa wa Mikoa, kanuniya 31 kipengele cha (11) na kanuni ya 39 kipengele cha (1) Brown Chalamila anafungi wa kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miezi kumi na mawili (12).