(Kulia),Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Bw. Oliva Paul Mhaiki na kushoto kwake ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Bw. Oliva Paul Mhaiki, amesema atapigania maslahi ya walimu nchini huku akiwataka walimu hao kutumiza wajibu wao ili kuboresha sekta ya elimu.