Simba Vs Yanga: Mashabiki waonywa kuhusu uwanja
Kuelekea katika mpambano wa watani wa Jadi Simba SC dhidi ya Yanga utakaopigwa siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mashabiki wa soka nchini wametakiwa kulinda mali za uwanja huo ili uendelee kudumu kwa matumizi ya baadaye.