Hatujatimiza malengo yetu Sudani Kusini - UN
Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS ambaye anamaliza muda wake Ellen Margrethe Løj amesema ameguswa sana na uvumilivu wa raia wa nchi hiyo lakini kinachomsikitisha ni kwamba matarajio yao kutokana na uhuru bado hayajatimia.