Jumanne , 29th Nov , 2016

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS ambaye anamaliza muda wake Ellen Margrethe Løj amesema ameguswa sana na uvumilivu wa raia wa nchi hiyo lakini kinachomsikitisha ni kwamba matarajio yao kutokana na uhuru bado hayajatimia.

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS ambaye anamaliza muda wake Ellen Margrethe Løj.

Bi. Løj amesema hayo mjini Juba, hii leo katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya kuondoka nchini humo wiki hii baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka miwili.

Amesema ilikuwa ni heshima kubwa kwa yeye kumwakilisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini akisema bado hawajakamilisha kazi yao kama umoja wa mataifa.

Bi Loj amesema kuwa mpaka sasa hakuna amani ya kutosha Sudan Kusini, hatuna ustawi lakini amewataka viongozi wa nchi hiyo kuweka ustawi wa wananchi mbele ili kuleta amani ya kudumu nchini humo.