Ijumaa , 24th Oct , 2025

Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Congo (DRC) Mhe. Felix Antoine Tshisekedi, umewasilishwa na Mjumbe Maalum na Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda wa nchi hiyo, Mhe. Floribert Anzuluni, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Congo (DRC) Mhe. Felix Antoine Tshisekedi, uliowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum na Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda wa nchi hiyo, Mhe. Floribert Anzuluni, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 24 Oktoba, 2025.