Mpinzani ashinda urais Congo DRC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Congo (Ceni) imetangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo yanayoonesha mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi ameshinda kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Desemba 30 mwaka uliopita.

