"Niko tayari kuwafundisha CCM" - Fatma Karume
Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika, TLS, Fatma Karume amesema yuko tayari kuitwa na chama chochote cha siasa nchini kwa ajili ya kutoa elimu ya masuala ya Katiba na sheria za nchi na kusisitiza kuwa msimamo wake hautabadilika.