Polisi Morogoro yadaka mtandao wa wizi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, linawashikilia watu 14 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukamatwa na vipande vya pembe za ndovu 13 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia moja thelasini na saba (137,576,250), pamoja na kukutwa na Gobole 4 zilizotengenezwa kienyeji.