PWANI: 'House boy' auliwa baada ya kuwaua watoto 2
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa amesema kuwa, bado wanachunguza ili kujua nini chanzo halisi kilichopelekea 'House Boy' kuwaua watoto wawili kwa kuwakatakata mapanga kwa madai ya kwamba, alikuwa na ugomvi na mama wa watoto hao ambaye na yeye alimjeruhi vibaya.

