"Wanasiasa ingieni kanisani mkinyenyekea" -Mndolwa
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglicana Tanzania, Maimbo Mndolwa, amewataka wanasiasa kuacha tabia ya kuingiza siasa kwenye nyumba za ibada, badala yake wayavue makoti yao ya siasa pindi wanapoingia kwenye nyumba hizo ili kuendelea kuidumisha amani iliyoachwa na waasisi wa nchi.

