Morrison matatani tena,Yanga kumchukulia hatua.
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kitendo cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na mchezaji wao Bernard Morrison katika mchezo wa jana wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Azam Sports Federation Cup waliolala kwa mabao 4-1 dhidi ya Simba watakichukulia hatua.

