Jumanne , 22nd Jul , 2014

Tuzo za muziki za Afrika za Jarida la African, zinatarajiwa kufanyika Jumamosi ya Tarehe 26 mwezi huu, ambapo wasanii Diamond Platnums, Lady Jay Dee, Ben Pol, Mrisho Mpoto na Sheddy Clever wamechaguliwa kuwania katika vipengele tofauti.

Tuzo za muziki za Afrika za jarida la African Afrimma

Sherehe za tuzo hizi zinatarajiwa kuwa za aina yake hasa kutokana na wasanii wakubwa Afrika, akiwepo Diamond Platnumz wa Tanzania, 2 Face, Davido na pia T-Pain kutoka Marekani kati ya wengine, kuwa katika orodha ya wasanii watakaopanda jukwaani kutumbuiza.

Hii inakuwa ni nafasi nyingine kubwa kwa muziki na wasanii wa Tanzania kupata nafasi ya kutangaza kazi zao katika ngazi ya kimataifa zaidi.