Alhamisi , 2nd Mar , 2017

Msanii wa bongo fleva Rama Dee amefunguka na kusema kuwa mtayarishajii wa video Hanscana kwa sasa yuko vizuri kuliko mkongwe kwa kazi hizo nchini Adam Juma na kwamba Adam Juma ana uwezo kuwa bora zaidi endapo atajifunza zaidi.

Kutoka kushoto: Hanscana, Adam Juma, Rama Dee

 
Rama Dee ametoa mtazamo wake huo kupitia ukurasa wake wa Instgram ambao baadhi ya mashabiki wamempinga na kusema kuwa amekosea sana kufanya hivyo huku wengine wakimuunga mkono.

"Adam Juma huyu dogo yupo vizuri kuliko wewe sasa hivi, Ila unaweza kuwa kama yeye au zaidi yake kama utajifunza zaidi! You know what I'm talking about Ma nigga" aliandika Rama Dee