Kocha wa zamani wa klabu ya Simba amesaini mkata wa kuitumikia timu ya Al Ahly Tripoli ya nchini Libya. Didie Gomes Da Rosa alikuwa akifundisha timu ya taifa ya Botswana kabla ya kujiuzulu nafasi yake na kutangazwa kwenye klabu hiyo ya Libya kuwa Kocha wao mkuu. Gomes raia wa Ufaransa alishinda taji la ligi kuu Tanzania bara, kombe la shirikisho Tanzania ( FA ) na aliiwezesha klabu ya Wekundu wa Msimbazi kucheza hatua ya robo fainali kombe la klabu bingwa Afrika msimu wa 2021.
Thomas Tuchel kocha wa zamani wa Chelsea ya England amesaini mkataba wa miezi 18 kuiongoza timu ya taifa ya England. Kikosi hicho mabingwa wa kombe la Dunia mwaka 1966 kilikua chini ya Kocha wa muda Lee Carsley baada ya aliyekua Mkufunzi mkuu wa timu hiyo Gareth Southgate kujiuzulu mwezi Julai 2024. Tuchel anakuwa Mwalimu wa tatu ambaye si raia wa Uingereza kuiongoza England baada ya Sven- Goran Eriksson na Fabio Capello. Mjerumani huyo aliyewahi kushinda tuzo ya Kocha bora Ulaya na Dunia mwaka 2021 atasaidiwa na Antony Barry aliyefanya naye kazi Chelsea na Bayern Munich.
Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United ameujia juu Uongozi wa Manchester United baada ya Mabosi wa klabu hiyo kumuondoa Sir Alex Ferguson kwenye nafasi yake ya Ubalozi wa Mashetani Wekundu wa Jiji la Manchester. Ferguson Kocha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya Mameneja wa Kingereza, aliiongoza Man U kushinda makombe 13 ya ligi kuu Uingereza, Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya mara mbili na Kombe la klabu bingwa Dunia msimu wa 2007-2008. Cantona alikuwa Mchezaji muhimu alitoa mchango mkubwa kwenye klabu ya Manchester United alishinda makombe ya ligi EPL mara 4 katika miaka 5.
Kuelekea dabi ya Kariakoo Oktoba 19, 2024 Beki kisiki wa timu Yanga Ibrahimu Abdullah Hamad maarufu kama Bacca amemtumia salamu Mshambuliaji wa timu ya Simba Lionel Ateba kwa kumwambia wataonana uwanjani tarehe 19. Ateba wiki iliyopita alizungumza kwenye siku ya Vyombo vya Habari kwa Timu za Ligi kuu Tanzania bara kwamba haoni Mlinzi wa kumzuia kufunga siku ya dabi kutoka kwenye kikosi cha Wapinzani wao siku hiyo kikosi cha Yanga kinachonolewa na Mwalimu Miguel Gamondi.
Daniel Maldini ameweka rekodi ya kuwa Mwanaukoo wa tatu kutoka Familia ya Wacheza Soka nchini Italia baada ya jana Oktoba 14, 2024 kwenye mchezo wa ligi ya Mataifa ya Ulaya dhidi ya timu ya Taifa ya Israel Daniel amefuata nyayo za Babu yake Cesare Maldini na Baba yake Paulo Maldini wote kuitumikia The Azzurri kwa vizazi vitatu tofauti.Cesare alianza kuitumikia Italia 1960,Paulo 1988 na Daniel 2024.
Timu ya Taifa ya Nigeria imepanga kugomea mchezo wa kufuzu AFCON 2025 Ugenini dhidi ya timu ya Libya. Kikosi cha Super Eagles kimeachwa uwanja wa Ndege kwa masaa 12 pasipo chakula wala maji ya kunywa, Wachezaji wamelazwa kwenye mabenchi ya Abiria huku mageti yakiwa yamefungwa na kutoa ugumu kwa timu ya Nigeria kuondoka uwanjani hapo.
Lamine Yamal amewastua Viongozi pamoja na Mashabiki wa Barcelona kuelekea mchezo wa La Liga dhidi ya Mahasimu Wao Wakubwa Real Madrid (El Clasico). Nyota huyo mwenye umri wa miaka 17 alitolewa nje ya Uwanja akiwa anachechemea kwenye mchezo dhidi ya Denmark muendelezo wa mechi za mashindano ya Mataifa Ulaya.
Mwanariadha wa Kenya mwenye umri wa miaka 30 Ruth Chepngetich ameweka rekodi mpya Chicago Marathon alitumia masaa mawili na dakika 9 na sekunde 57 na kuvunja rekodi iliyowekwa na Assefa mwaka 2023 ambaye alikimbia mbio ndefu kwa masaa mawili dakika 53 na sekunde 53. Chepngetich pia amewahi kushinda ubingwa wa Dunia mwaka 2019.
Bondia wa Australia amefanikiwa kutetea ubingwa wake wa WBC uzito wa Unyoya baada ya kupata ushindi wa pointi kutoka kwa Majaji walioshuhudia pambano hilo. Pambano la kwanza la ubingwa kwa uapande wa Wanawake kufanyika nchini Saudi Arabia limetizamwa kama ni hatua chanya kwa Taifa hilo kwenye michezo kwa upande wa Wanawake na tunaweza kuanza kushuhudia Mabondia Wakike kutoka Saudi Arabia wakipambana ulingoni.
Nahodha wa Ureno Criastiano Ronaldo amefunga goli lake la 133 akiwa na jezi ya timu ya Taifa lake kwenye mchezo waliocheza ugenini dhidi ya Poland siku ya jana Oktoba 12, 2024, kumfanya aendelee kuiweka vizuri rekodi yake ya kuwa Mchezaji aliyefunga goli nyingi kwenye michezo rasmi ya kimataifa kwa upande wa Wanaume. Kwenye ushindi dhidi ya Poland Ronaldo amefikisha goli la 903 tangu aanze kucheza soka.
Taifa Stars inashika nafasi ya pili kwenye kundi H nyuma ya Congo DRC yenye alama 9 ikiwa imecheza michezo mitatu sawa na idadi ya Stars iliyojikusanyia alama 4 iliyo nafasi ya pili. Timu ya taifa ya Tanzania imepoteza mchezo ugenini dhidi ya Congo DRC kwa goli 1-0, mchezo wa marudiano wa kufuzu michuano ya AFCON 2025 unatarajiwa kuchezwa Oktoba 15, 2024 Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam.
Nahodha wa timu ya timu ya taifa ya Ureno ameitumikia timu hiyo michezo 214 akifunga goli 132. Akiwa amedumu kwenye timu hiyo mabingwa wa ubingwa wa mataifa ya Ulaya UEFA EURO 2016,kwa miaka 20 Ronaldo ndiye Mchezaji bora wa Ureno wa muda wote mbele ya Eusebio na Luis Figo japo kwa sasa Mashabiki wanataka apumzike apishe damu changa
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo Oktoba 10,2024 itashuka dimbani ugenini dhidi ya Congo DRC kweye mchezo wa kufuzu mashindano ya AFCON itakayofanyika nchini Morocco 2025. Stars itaingia kwenye mchezo huu ikichagizwa na urejeo wa Nahodha wa timu Mbwana Samatta ambaye alikosekana katika michezo miwili iliyopita ya timu ya taifa.
Klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga imehamia mkoani Arusha na itatumia uwanja wa itaufanya uwanja wa Sheik Amri Abedi kuwa uwanja wake wa nyumbani kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara kipindi chote ambacho uwanja wa Mkwakwani unaendelea kufanyiwa matengenezo. Awali timu hiyo Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara mwaka 1988 ilikua inautumia uwanja wa KMC Complex kama uwanja wake wa nyumbani.
Jina Beki kisiki wa klabu ya Arsenal ya Uingereza limeibuka kwenye listi ya Florentino Perez Real ambao anataka kuwasajili pindi dirisha kubwa litakapofunguliwa majira ya kiangazi, William Saliba anatajwa kama mmoja wa Walinzi bora wa kati kwa sasa Duniani Raisi wa Los Blancos anaona Saliba atakuwa tiba ya safu ya Ulinzi ya mabingwa hao watetezi wa La Liga kwa muda mrefu
