Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United ameujia juu Uongozi wa Manchester United baada ya Mabosi wa klabu hiyo kumuondoa Sir Alex Ferguson kwenye nafasi yake ya Ubalozi wa Mashetani Wekundu wa Jiji la Manchester. Ferguson Kocha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya Mameneja wa Kingereza, aliiongoza Man U kushinda makombe 13 ya ligi kuu Uingereza, Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya mara mbili na Kombe la klabu bingwa Dunia msimu wa 2007-2008. Cantona alikuwa Mchezaji muhimu alitoa mchango mkubwa kwenye klabu ya Manchester United alishinda makombe ya ligi EPL mara 4 katika miaka 5.
Nahodha wa zamani wa Manchester United Eric Cantona ameujia juu Uongozi wa sasa wa klabu hiyo kutokana na kitendo cha kumuondoa Sir Alex Ferguson katika nafasi ya Ubalozi wa klabu hiyo, kwa kuuita uamuzi huo ni kumkosea heshima Kocha huyo ambaye Wapenzi wengi wa Soka wanamuona ndiye kocha bora wa muda wote wa klabu za mpira wa miguu Duniani.
Cantona alifanya kazi na Ferguson kuanzia mwaka 1992, alisajiliwa na Kocha huyo raia wa Scotland kutoka klabu ya Leeds United. Kwa pamoja walishinda makombe manne ya Ligi ya Uingereza ndani ya miaka mitano.
Nyota huyo raia wa Ufaransa aliyesifika kwa ukorofi kipindi cha uchezaji wake amezungumza kwa uchungu mkubwa kuhusiana na kuondolewa kwake kocha wake wa zamani kwenye nafasi yake ya Ubalozi wa heshima wa United. Eric amesema Uongozi huo hauna heshima na hauthamini kabisa alama aliyoiweka Mscotland huyo ndani ya klabu hiyo.
Mashabiki wa Mashetani Wekundu wengi pia wameonyeshwa kuchukizwa na uamuzi huo kwa kusema Uongozi wao unapaswa kuondoa Wachezaji wasio na mchango katika timu yao na kuacha kutafuta sababu zisizo za msingi za kubana matumizi.
Taarifa rasmi ya klabu ilisema Sir Alex Ferguson hatokuwa sehemu ya Uongozi wa klabu hiyo katika nafasi aliyokua anaitumikia mwishoni mwa msmu huu wa 2024-2025, kutokana na umri wake ambapo atatimiza miaka 83 mwezi Disemba 2024.
Sir Alex Ferguson alijiunga na Mnchester United mwaka 1986 na aliitumikia klabu hiyo mpaka mwaka 2013 alipostaafu. Mscotland huyo aliiwezesha Mnchester United kufuta utawala wa Liverpool kwenye ligi kuu Uingereza kwa kipindi cha miaka 26 alichokaa United alishinda Ubingwa wa ligi Uingereza mara 13, FA mara 5 pamoja na kombe la ligi ya mabingwa Ulaya mara 2 mwaka 1999 na 2008.