Mwanamuziki wa bendi mpya nchini ya Stars Band, Anneth Kushaba
Anneth amesema wimbo huo ambao upo katika mahadhi ya Pop utawafanya Watanzania wajue sio kila Band inapiga mtindo unaofafana, hivyo mwanzo wa wimbo huo ni mfululizo wa nyimbo nyingine kutoka kwa band hiyo.
Anneth amesema kuwa kwa sasa tafrani ya nani mmiliki wa band hiyo imeshakwisha na ipo chini yake hivyo wimbo huo utakua maalumu kwa ajili ya kuitambulisha band kwa wadau rasmi.