Jumatatu , 18th Apr , 2016

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini imesema inalenga kutokomeza kiwango cha maambuki ya maralia kutoa asilimia 18 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 1 ifikipo mwaka 2020.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro Jana

Akizungumza katika sherehe za uwashwaji wa Mwenge mkoani Morogoro, Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema juhudi hizo za serikali zinafanywa kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti maralia chini ya Wizara ya Afya, ambao una kauli mbiu ya wekeza kwa maisha ya baadaye tokomeza Maralia.

Mhe Samia amesema Ugonjwa wa Maralia hapa nchini bado ni tishio kwa wananchi na kuwataka watanzania kuchukua hatua za kujilinda wenyewe ikiwa ni pamoja na kutumia chandarua pamoja na kutokomeza mazalia ya mbu.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amesema kuwa licha ya kujikinga na maralia, wasisahau maambukizi ya virusi vya UKIMWI bado yanaendelea hivyo wananchi hawana budi kuchukua hatua ya kujikinga na ugonjwa huo.

Amesema kuwa ugonjwa huo bado unapunguza nguvu kazi ya taifa hivyo serikali imeamua kuanzisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo ambao kauli mbiu ya mwaka huu itakuwa ni “Tanzania bila maambukizi mapya , unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana.